
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2022, jumla ya kondomu 111,934,600 zilisambazwa nchini ili kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, huku kati ya hizo, kondomu 2,806,500 zilisambazwa katika Wizara na Taasisi mbalimbali.
.
Dkt.Mollel, ameyasema hayo, wakati akiwasilisha taarifa kuhusu kuhuisha na kujumuisha maswala ya UKIMWI mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI.
