Back to top

JWTZ yaonya wananchi kutovamia maeneo ya Jeshi.

11 July 2020
Share

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaonya  wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya mazoezi ya kijeshi kuacha tabia ya kuvamia maeneo hayo kwakuwa wanakwamisha shughuli za jeshi na kuhatarisha usalama wao kwakuwa maeneo hayo ni maaalum kwaajili ya mazoezi ya silaha za kijeshi

Mkuu wa mafunzo mtandaji kivita wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jeneral  Alfredy Kapinga ametoa kauli hiyo wilayani Monduli mkoa wa Arusha katika hitimisho la  zoezi la medani kwa onesho la shambulio la kunuia mchana lililohusisha silaha nzito za kivita vikiwemo vifaru, rocket ranger, mizinga pamoja na zingine kwa zaidi ya askari  wanafunzi  mianne  kundi maalum la nne mwaka 2020.

Mkuu wa shule ya awali ya mafunzo ya kijeshi ya RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala amesema vijana hao  wa kundi maalum waliofanya vizuri kwenye mchepuo wa sayansi watasaidia kulibadilisha jeshi la Tanzania.