Back to top

KALEMANI amemwagiza Mkandarasi kusambaza umeme wa vijini.

21 April 2018
Share

Waziri wa Nishati Dakta MENDRAD KALEMANI amemwagiza Mkandarasi wa kampuni ya Sengerema Engeneering Group inayojenga njia ya kusambaza umeme wa vijini - awamu ya tatu Mkoani Iringa kukamilisha zoezi hilo katika muda uliopangwa.

Waziri KALEMANI pia amewahakikishia wanachi kuwa serikali imedhamiria kutoa huduma hiyo ya umeme kulingana na mahitaji.

Amesema hayo katika ziara yake Mkoani Iringa kukagua maendeleo ya mradi huo na kukutana na wananchi katika Kijiji cha Mibikimitali, Wilayani Iringa na Kinyanambo Wilayani Mufindi.

Baadhi ya wananchi katika kijiji hivyo wameiomba serikali kuusimamia mradi huo kwa karibu ili ukamilike  haraka na kutoa huduma na tija.

Zoezi la kusambaza umeme wa vijijini linatarajiwa kukamilika mwaka 2021 ambapo zaidi ya vijiji Elfu Kumi vinatarajiwa kufikiwa na huduma hiyo nchi nzima.