Back to top

KAMANDA MALLYA:WATUMIENI ASKARI KUSINDIKIZA FEDHA 

12 December 2023
Share

Wafanyabiashara wakubwa wilayani Songwe, wametakiwa kuwachukua askari kwa ajili ya kuwasindikiza (Escort) wanapokuwa kwenye shughuli zao za kwenda kuuza madini na kuchukua hela na kupeleka hela bankI ili kuepuka kufanyiwa uhalifu wanapokuwa njiani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya ameyasema hayo, wakati akifungua mafunzo ya ulengaji wa shabaha kwa wamiliki wa silaha za kiraia wilaya ya Songwe ambapo ameongeza kuwa ni vyema wanapokwenda kupima dhahabu au wanapokuwa na fedha nyingi ni bora wachukue askari kwa usalama wako na mali yako.

“Unakuta mtu anaenda kupima dhahabu au kupeleka hela benki bila ulinzi kutokana na hivyo anavamiwa na kuchukuliwa hela pamoja na mali zake mara nyingine na yeye anapoteza uhai kwa jambo ambalo angefuata utaratibu wa kuchukua askari Polisi kwa ajili ya ulinzi madhara hayo yasingeweza kutokea” alisema Kamanda Mallya.