
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw.Joseph Mkirikiti amesema mkoa huo umeanzisha kampeni ya kukabiliana na ugonjwa wa wa polio kwa kutoa chanjo nyumba kwa nyumba kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, baada ya ugonjwa huo kujitokeza katika nchi jirani ya Malawi.
Mkirikiti ametoa kauli hiyo katika kikao cha kampeni ya kudhibiti ugonjwa huo kuwa kutokana na mwingiliano uliopo baina ya nchi hiyo Tanzania na Malawi, serikali imetoa chanjo itakayotolewa nyumba kwa nyumba kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Amewaagiza maofisa afya wahakikishe elimu inafika kwa wazazi na walezi kuhusu athari juu ya ugonjwa huo.
