Back to top

KAMPENI ZA UCHAGUZI KENYA ZILIKUWA ZA AMANI

11 August 2022
Share

Kiongozi wa Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya, kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kampeni za uchaguzi nchini Kenya zilikuwa za amani, licha ya matukio machache ya vurugu ambayo yalishughulikiwa na vyombo vya usalama.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema matukio hayo hayakuondoa taswira nzima ya uchaguzi nchini humo, huku akiipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo kwa kuratibu vyema zoezi la uchaguzi.

Mheshimiwa Kikwete amevipongeza vyombo vya habari kwa kutoa habari sahihi na kuzima habari za uzushi katika zoezi la utoaji matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Kenya.

Amesema ujumbe wao ulibaini baadhi ya mitandao ya kijamii ilitumika kusambaza taarifa za uongo na chuki.