
Baadhi ya Wananchi kwenye maeneo mbalimbali leo wamejitokeza kupiga kura kuwachagua madiwani wao kkatika uchaguzi mdogo wa kata 22 za Tanzania Bara.
Kata zinazofanya uchaguzi ni Kata zinazofanya uchaguzi ni Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Mshikamano (Halmashauri ya Manispaa ya Musoma), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).
Kata nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu), Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).
