Back to top

KATAMBI APONGEZA POLISI KUPAMBANA NA UHALIFU

11 February 2026
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi amelipongeza Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kwa kupambana na uhalifu, hali iliyopelekea kupungua kwa matukio 746 ambapo matukio 3091 yaliripotiwa mwaka 2024 huku mwaka 2025 yakiripotiwa matukio 2345.

Akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani humo, Waziri Katambi alizungumzia pia kulindwa kwa watalii akikumbushia jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi, katika kuutangaza na kuukuza utalii.

Masuala mengine aliyozungumzia ni Mauaji yanayotokana na watu kujichukulia Sheria mkononi, Makosa ya Barabarani yanayosababishwa na watumiaji wa vyombo vya moto kutofuata sheria za Usalama Barabarani.