Back to top

KAULI YA JESHI LA ISRAEL KWA WAPALESTINA, YAIBUA HOFU

13 October 2023
Share

Hofu na mkanganyiko umeibuka huko Gaza, baada ya Jeshi la Israel kuwaambia zaidi ya Wapalestina milioni 1 waliokwama Kaskazini mwa eneo lililozingirwa kuhamia Kusini, ndani ya saa 24 kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa.

UN inasema uhamishaji wa watu wengi "haiwezekani", unaweza kuwa na matokeo mabaya. 

Hamas imeliita tamko hilo la Israeli kuwa ni "propaganda bandia", na imewaambia wakazi kupuuza maneno hayo.

Takriban Wapalestina 1,537 wameuawa na 6,612 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza huku idadi ya watu waliouawa nchini Israel imefikia 1,300.