Back to top

Kaya 15 zaishi kwenye mahema Tanga.

14 January 2020
Share

Zaidi ya kaya kumi na tano zenye watu zaidi ya mia moja zinalazimika kuishi kwenye mahema chini ya mti baada ya nyumba zao kubomolewa huko wilayani Kilindi mkoani Tanga.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Kilindi amesema watu hao wamevunjiwa kutokana na amri ya mahakama lakini pia diwani wa kata ya Kilindi amedai kuwa kwa sasa wanawatafutia eneo jingine wananchi hao.