Kenya imepiga marufuku mikutano ya hadhara kwa sababu ya Corona.

Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amethibitisha kutokea kwa kisa cha kwanza cha virusi vya Corona nchini humo.

Kenya imepiga marufuku mikutano ya hadhara,ziara zote kwenye magereza ya Kenya zimepigwa marufuku na mikutano kwenye shule nchini Kenya imepigwa marufuku.

Mkenya aliyepatikana na kirusi cha Corona alikuwa anatoka Marekani jimbo la Ohio akapitia Chicago, Uingereza kisha Kenya na alifika Kenya Machi 5 mwaka huu.