
Kenya imepokea shehena ya kwanza dozi millioni 1.02 ya chanjo ya Corona ya Oxford AstraZeneca kutoka shirika la COVAX.
Chanjo hiyo imepokewa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe ikisafirishwa na ndege ya shirika la ndege la Etihad ikitokea Doha Qatar.
Kulingana na Kagwe wahudumu wa afya ndio watakaochanjwa wa kwanza kisha maafisa wa usalama na waalimu.
Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga watajakuwa wa kwanza katika hospitali ya Kenyatta ijumaa.