
Serikali ya Kenya imesema inachelewesha kufungua tena mpaka wake na Somalia, baada ya mashambulizi katika ardhi yake, yanayohusishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al-Shabab.
Hayo yemeelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki, kuwa uamuzi huo umetokana na matukio ya hivi majuzi ya vitisho na visa vya ukosefu wa usalama katika kaunti za mipakani, hivyo awamu za kufunguliwa upya kwa mpaka kwenye mpaka mrefu hazitaendelea kama ilivyotangazwa mwezi Mei.
Waziri Kindiki alitangaza kuwa baada ya wiki chache Kenya, itaanza kuwaunganisha wakimbizi ambao wamekuwa wakiishi kambini, kama sehemu ya njia mpya ya kuwadhibiti.
