
Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli nchini kenya (EPRA) imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zitaanza kutekelezwa kuanzia kati ya Aprili 15 na Mei 14, 2022 huku ikionyesha bei ya bidhaa hiyo imeongezeka kwa shilingi 9.90, ambapo kulingana na Mamlaka hiyo mafuta ya petroli sasa yatauzwa kwa Sh144.62/- kwa lita, dizeli shilingi 125/- kwa lita huku mafuta taa yakigharimu Shilingi 113.44/- kwa lita.
.
Bei hizo mpya za mafuta zinatangazwa huku kukiwa na uhaba wa bidhaa hiyo nchini humo.
.
Hata hivyo, Waziri wa Kawi Monicah Juma amesema kuwa usambazaji shwari wa mafuta unatarajiwa baada ya saa 72 huku akiwaonya watakaobainika kusababisha uhaba wa bidhaa hiyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
