Back to top

Kenyatta awapa mawaziri na makatibu mapumziko ya lazima.

15 August 2020
Share

Rais Uhuru Kenyatta amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko ya lazima huku kukiwa na taarifa za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri hivi karibuni.

Kupitia barua kwa mawaziri na makatibu wa wizara iliyotumwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua likizo hiyo ya siku 11 itaanza Jumatatu, Agosti 17 hadi Agosti 28 kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Rais jijini Nairobi. 

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa mawaziri na makatibu watahitajika tu kushughulikia  majukumu ya dharura.

Likizo hiyo ya mawaziri na makatibu anakuja huku kukiwa kuna taarifa kuhusu Rais Kenyatta kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri huku tetesi zikidai atahusisha zaidi viongozi kutoka upinzani serikalini.