Back to top

Kesi ya kupinga matokeo nchini Malawi yaanza kusikilizwa.

09 August 2019
Share

Mahakama ya kikatiba nchini Malawi imeanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambayo ilifunguliwa na upinzani nchini humo miezi mitatu iliyopita.

Kesi hiyo ilifunguliwa na chama kikuu cha upinzani cha nchini humo MCP ikidai kuwa kulikuwa na vitendo vya udanganyifu katika uchaguzi wa Rais uliofanyika Mei 21 ya mwaka huu.

Kiongozi mkuu wa upinzani Lazarus Chakwera amesema kuna udanganyifu ulifanywa na Rais wa sasa wa nchi hiyo Peter Mutharika ambaye alishindwa uchaguzi huo ambapo kura laki moja na elfu hamsini na tisa alizopigiwa Chakwera ziilibwa na kambi ya Mutharika.

Wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo kulikuwa na ulinzi mkali nje ya mahakama huku kukiwa na vikundi kadhaa vya watu nje ya mahakama hiyo vikifuatilia muenendo wa kesi.