Back to top

Kesi ya Mbowe: Shahidi aliyeugua akitoa ushahidi apona.

18 January 2022
Share

Shahidi wa kumi katika kesi ya uhujumu uchumi na vitendo vya kigaidi upande wa Jamhuri inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake Inspekta Innocent Ndowo baada ya kuugua ghafla hapo jana wakati akitoa ushahidi wake amepona na leo anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa serikali Pius Hilla, kutambua vielelezo vya simu nane alizodai kuzifanyia uchunguzi wa kitaalamu katika ofisi ya Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi makao makuu ya Jeshi la Polisi.