Back to top

Kesi ya Mbowe:Pingamizi la kitabu cha mahabusu yatupiliwa mbali.

22 November 2021
Share


Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi ya kutaka mahakama hiyo ikatae kupokea kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu kutoka Kituo Kikuu cha Polisi kati jijini Dar es Salaam baada ya hoja tatu za upande wa utetezi kukosa mashiko.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga wakati akisoma uamuzi wa pingamizi hiyo na kusema kielezo hiko kinapaswa kupolelewa na mahakama kwa kuwa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo alitoa kielezo hicho kama utambuzi na sio maombi ya kutaka mahakama kupokea kieleezo hicho cha kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu.