Back to top

KIBANO MAKANDARASI WANAOFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO

08 May 2024
Share

Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imesema inaanza operesheni maalum kukagua miradi mikubwa inayotekelezwa na Makandarasi kutoka nje ya nchi, kutokana na miradi mingi kusuasua na kutekelezwa chini ya viwango. 

Hayo yamebainishwa Jijini Arusha na Msajili wa CRB, Rhoben Nkori, nakueleza kuwa bodi hiyo imeamua kufanya operesheni hiyo maalum kuanzia mwezi Mei hadi katikati ya mwezi Juni mwaka huu, kufuatia ziara mbalimbali za Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa katika miradi mbalimbali ikiwemo barabara ambayo imeonekana thamani yake kuwa ndogo.

Bw.Nkori amewataka Makandarasi wote kutambua kuwa operesheni hiyo maalum itafanyika hadi mwezi Juni, 2024 kujiridhisha wakandarasi wote walioingia mkataba na serikali kama wanafanya kwa mujibu wa mikataba waliyoingia, kinyume na hapo hatua zitachukuliwa.

"Baada ya kufuatilia ziara ya Waziri tumeamua kama Bodi kupitia miradi hii na kujifunza utekelezaji thabiti kwa wakandarasi waliofanya vizuri ili kujifunza mbinu walizotumia ili zisaidie kutumia kwa wakandarasi wazawa, kikubwa zaidi kwenda kupitia na kuangalia makandarasi hawa ambao wanafanya kazi kwa kusuasua na tumewasajili wakiwa ni wakandarasi wakubwa ni kwanini wanafanya miradi chini ya kiwango au kufanya kinyume na tutakagua tukijiridhiishisha wakandarasi hawa kazi wanazofanya haziendani na mikataba waliyoingia na kama sheria yetu itaturuhusu kuchukua hatua kwa kuwaondoa kwenye usajili kama ambavyo tuliwaingiza"Amesema Nkori.

Meneja wa CRB Kanda ya Kaskazini, Sauda Njila amesema mafunzo hayo ya siku tatu yatakutanisha wadau 150 ambapo mafunzo hayo ya usimamizi wa fedha yatasaidia sekta hiyo ya ujenzi hapa nchini hasa wa Makandarasi wazawa.

Amesema mafunzo hayo hutolewa kufuatia tafiti mbalimbali ambapo wamebaini Makandarasi wakipata mafunzo mbalimbali yatawasaidia
kuboresha utendaji kazi wao na kuwa na matokeo mazuri.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makandarasi na watoa huduma ShirikishiTanzania (TUCASA), Mhandisi Yahaya Mnali, alisema mafunzo hayo ni muhimu na yana manufaa kwani yatasaidia kuboresha fani hiyo na
kutekeleza wajibu wao kikamilifu.