Kikosi cha doria cha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Simiyu na Magu kimekamata kilo 951 za samaki wadogo aina ya sangara wenye thamani ya shilingi milion tatu ambao wamevuliwa kinyume cha sheria ya uvuvi namba 22,2003.
.
Kufuatia kukamatwa kwa samaki hao Afisa Usimamizi wa doria kanda ya Simiyu na Magu Hamad Stima ametoa wito kwa wavuvi na wafanyabiashara ya samaki kufuata sheria za uvuvi na kuacha kujihusisha na uvuvi haramu.