
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.DKT.Selemani Jafo, ametoa agizo hilo wakati akikagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Anglo De Beers, kilichoko Mwaoga Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Mhe.Jafo amempongeza mwekezaji huyo kwa kuanza kujenga miundombinu ya kuhifadhi mazingira kabla kuanza kwa shughuli za uchimbaji kama sheria na kanuni zake zinavyoelekeza na kueleza kuridhishwa na namna mwekezaji huyo alivyojipanga katika uzalishaji wa madini hayo hasa hasa kwa kuchimba bwawa la tope sumu ambalo atahifadhi majitaka na ametaka wengine waige mfano huo.
Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji ukiwemo wa madini lakini wawekezaji hao pamoja na kuwa na mtu wa kusimamia usalama wa wafanyakazi wanapaswa pia kuzingatia kulinda mazingira.
