Back to top

KILIMO CHA VANILLA MKOMBOZI WA AJIRA KWA VIJANA

21 September 2022
Share

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kusini Visiwani Zanzibar, wamesema uwepo wa mradi wa kilimo cha zao la Vanilla umesaidia kuongeza ajira kwa vijana na kupunguza kilio cha ajira kwa vijana.
 
Wakizungumza na ITV baadhi ya vijana wanaofanya kazi katika mashamba ya Vanilla, wamesema mradi huo umewapatia ajira za kudumu na kuwafanya kukidhi mahitaji yao na mahitaji ya familia zao na kuondokana na kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa ajira.