Back to top

KILIO CHA TOZO, SERIKALI YAFUTA TOZO KWENYE MIAMALA YA KIELEKTRONIKI

20 September 2022
Share

Serikali imefuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda kwenye mitandao ya simu na kufanya marekebisho ya tozo mbalimbali za Kielektroniki.

Akitoa kauli ya serikali Bungeni Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Mwigulu Nchemba, amesema hatua hiyo inazingatia maoni ya wananchi na agizo la kamati kuu ya chama cha mapinduzi.

Amesema serikali pia imefuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine au kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

Aidha serikali imetoa msamaha kwenye tozo ya miamala kwa kupunguza  gharama ya miamala kwa asilimia 10 kw amakundi ya maiamala kwa kuzingatia gharama za makundi.

Mhe.Mwigulu amesema hatua hizo zitaanza  kutekelezwa tarehe moja Oktoba 2022, kutoa nafasi kw amarekebisho ya mitambo.

Aidha serikali imefanya makerekebisho kwenye kodi ya zuio ya pango la majengo ambayo sasa italipwa na mwneye nyumba na sio mpangaji kupitia mamlaka ya mapato TRA.

Mh.Mwigulu ameliambia bunge fedha hizo zitafidiwa kwenye bajeti kwa kubana matumizi mengine ya serikali yasiyoathirii miradi ya maendeleo .