Back to top

KILO 980 ZA SAMAKI WALIOVULIWA KWA BARUTI ZAKAMATWA

24 January 2023
Share

Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji Dar es salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Mifugo, limewakamata watu wawili wakiwa na samaki Kg.980 zilizokuwa ndani ya boti yenye usajili namba Z.103585 yenye jina MV.MAEDRA, wakituhumiwa kuvua samaki hao kwa kutumia baruti, ambapo limebainisha kuwa taratibu za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani zinaendelea.