Back to top

Kim Jong Un: Tutaendelea kufanya majaribio ya makombora

28 March 2022
Share

Rais wa Korea Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesema nchi yake itaendelea kutengeneza silaha nzito za kivita yakiwemo makombora ambapo amesema mbinu pekee ya kukwepa vitisho kutoka kwa Mabeberu ni kujiimarisha kwa kutumia silaha nzito za kivita huku akisisitiza kuwa ataendelea kufanya majaribio na hata ikibidi kufanya jaribio la silaha za nyuklia.