Back to top

KIMBUNGA FREDDY CHAUA WATU 200 MALAWI

15 March 2023
Share

Idadi ya watu waliofariki dunia nchini Malawi kutokana na Kimbunga Freddy imefikia 200, eneo la Kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja. 

Mvua inaendelea kunyesha hali ambayo imeleta ugumu kwa waokoaji kuhangaika kutafuta maiti na walionusurika kwenye tope. 

Inakadiriwa watu 19,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo.

Aidha Mamlaka ya elimu nchini Malawi ililazimika kuchukua tahadhari kwa kuzifunga shule katika Wilaya 10, kutokana na wasiwasi wa usalama baada ya Kimbunga Freddy kusababisha uharibifu katika nchi jirani ya Msumbiji.