
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu, amesema Wizara yake itaendelea kutoa kipaumbele na kuwalinda wazalishaji wa dawa na vifaa tiba waliopo hapa nchini, ili kuongeza uzalishaji pamoja na ukuaji wa uchumi.
Waziri Ummy ameeleza hayo alipokutana na kufanya kikao na Wazalishaji na Wasambazaji wa Bidhaa za Afya (Dawa na Vifaa tiba) nchini, kujadili changamoto na fursa za Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati zaidi ya kukuza wawekezaji hao nchini, ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo pamoja na kulinda Viwanda vya ndani.
Wazalishaji Dawa na Vifaa tiba lazima mjipange, tusije tukaweka vikwazo kwa viwanda vya nje kuleta bidhaa hapa nchini ili hali hamna uwezo wa kuzalisha bidhaa bora na kumudu soko la hapa nchini hilo suala TMDA nawaachia mliangalie mtuletee majibu” amesema Ummy Mwalimu
Ni lazima tuangalie suala la kulinda viwanda vya ndani vya dawa na vifaatiba, hawa wamewekeza hata kama wanazalisha kidogo tunatakiwa kuwalinda kwa kutoa kipaumbele kwao kwenye ununuzi wa dawa na vifaatiba vya ndani ya nchi”amesema Ummy Mwalimu kwenye kikao na Wazalishaji Dawa
