Back to top

KIPINDUPINDU CHAUA WATU 10 AFIKA KUSINI

22 May 2023
Share

Watu takribani 10 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu, katika jimbo Gauteng lenye watu wengi zaidi nchini Afrika Kusini.

Jumatatu iliyopita watu 95 walifikishwa hospitali wakiwa na dalili za kipindupindu huko Hammanskraal, kaskazini mwa mji mkuu, Pretoria.

Mkuu wa Afya wa Mkoa, Nomantu Nkomo-Ralehoko, amewataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi na kudumisha usafi.