Back to top

KITUO CHA AFYA CHASHINDWA KUTOA HUDUMA KISA KICHOMEA TAKA

22 November 2022
Share

Kituo cha Afya Ndola kilichopo wilayani Ileje mkoani Songwe kilichogharimu kiasi cha shilingi Mil.381 zilizotokana na tozo za miamala ya simu, kimeshindwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi, baada ya kituo hicho kukosa kichomea taka(incinerator) na kupelekea wakazi wa eneo hilo kutembea zaidi ya kilometa 15 kufuata huduma za afya wilayani.
.
Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi.Happines Seneda amewataka viongozi waliopewa jukumu la kusimamia mradi huo kuhakikisha unaanza kutoa huduma haraka iwezekanavyo.