Back to top

KITUO CHA POLISI CHATELEKEZWA KIKIWA HATUA YA UJENZI SONGWE

02 February 2023
Share

Kituo cha Polisi Kata ya Mpona, iliyopo wilayani Songwe kinachojengwa kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na serikali pamoja na  mfuko wa jimbo kilichoanza kujengwa tangu mwaka 2016, kimetelekezwa kikiwa katika hatua ya ujenzi ambapo baadhi ya wasimamizi wa ujenzi, huo wakituhumiwa kwa upotevu wa vifaa ikiwemo mifuko 50 ya Saruji, huku wananchi wa eneo hilo wakiingia hofu ya usalama wao baada ya kukithiri kwa matukio mbalimbali yakiwemo mauaji.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata hiyo Bw.Marco Aloyce, mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo.