Back to top

KITUO KIPYA CHA AFYA KUJENGWA KATIKA KIJIJI CHA GENDABI

29 December 2023
Share

Serikali imesema itajenga kituo kipya cha Afya katika Kijiji cha Gendabi, kilichopo wilayani ya Hanang mkoani Manyara ili kusaidia upatikanaji wa huduma za Afya, karibu na wananchi. 
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, alipotembelea na kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ambapo pia alitoa pole kwa wananchi walioathirika na maporomoko ya matope.
.
Waziri Ummy, amesema katika kutekeleza ujenzi wa Kituo hicho cha Afya wataanza na Tsh. Mil. 500/=, na kwamba Kituo hicho  kitajengwa katika eneo la makazi mapya yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi waliothirika na maporomoko hayo.
.
Aidha Waziri Ummy amesema watapeleka magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwenye Wilaya hiyo ambapo amefafanua kuwa magari hayo, sio yale ya mgao yaliyonunuliwa na Rais Samia, zaidi ya 900, ambayo TAMISEMI watayapeleka.