
Kiwanda kinachohusika na utengenezaji wa Magodoro, Furniture pamoja na Mitungi ya Gesi cha Ocean Kiss kilichopo Tabata Bonde la Sukita jijini Dar es Salaam kimewaka moto.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Sukita wamesema moto huo umeanza majira ya saa tatu asubuhi tarehe 19 April 2018 ambapo kumekuwepo na milio ya milipuko ambayo inasababishwa na gesi jambo ambalo limesababisha taharuki kwa wakazi waliopo eneo hilo.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la zimamoto na uokoaji limepiga kambi tayari eneo hilo ilikuweza kukabiliana na moto huo ambao umezuka ambao bado unaendelea kuwaka.
Mwandishi wetu aliyepo eneo hilo ametujuza kwamba chanzo cha moto huo kimefahamika kuwa kinatokana na cheche zilizotokana na uchomeleaji uliokuwa ukifanyika katika kiwanda hicho.
Awali chanzo cha moto kilikuwa hakijafahamika mara moja, madhara yaliyotokana na moto huo bado hatujafahamu lakini tutawajuza kadri mwandishi wetu anavyozidi kuzipata katika eneo hilo.
Zaidi fuatilia hapa.