Back to top

Koboko amng’ata mtoto Songwe,afariki baada ya dakika 48.

17 May 2019
Share

Nyoka aina ya Koboko amemng'ata mtoto Pelanji wa miaka 4 mkazi wa kijiji cha Masanyinta kata ya Mpapa wilaya ya Momba mkoani Songwe, ambaye amefariki dakika ya 48 baada ya sumu kusambaa mwilini.

Mtaalamu wa masuala ya tabia za wanyamapori Bi. Janneth Masembo amesema Koboko ni nyoka mwenye sumu 2 zinazoweza kuua mtu kwa dakika 24 kama majeruhi akichelewa matibabu.

Amesema, majeruhi anaweza kuchelewa kufariki kwa sababu ya kuwa na kinga imara ya mwili iwapo tu ameng'atwa sehemu tofauti na utosini.

Ameeleza kuwa Koboko ni nyoka hatari mwenye aibu, lakini akikasirishwa ana uwezo wa kuua idadi kubwa ya watu kwa kasi na ndani ya muda mfupi.

Isaac Benithet mkazi eneo hilo amejitosa peke yake akawatawanya watu waliokuwepo eneo la tukio na kupambana na koboko ndani ya saa moja na kufanikiwa kumuua.