Back to top

Kocha wa Al Ah Ahly Pitso Mosimane aimwagia sifa Simba.

22 February 2021
Share

Ikiwa ni siku moja tu kabla ya mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi kati ya Simba dhidi ya Al Ahly hatimaye kocha wa Al Ahly raia wa Afrika kuamini Pitso Mosimane amesema amevutiwa na Simba kupata matokeo ugenini dhidi ya AS Vita.

"Navutiwa sana na Simba kwa kwenda Kinshasa  na kushinda dhidi ya Vita na hicho ni moja kati ya vitu muhimu tunahitaji kuwa makini dhidi ya Simba".

"Walicheza vizuri sana kwa ushirikiano kuonesha kazi ya mwalimu wao na benchi lao la ufundi liko vizuri zaidi".

"Simba pia ni timu inayocheza kwa nguvu ya mashabiki wanapenda kuona mpira mzuri wana timu yenye kuwafurahisha na yenye furaha".

"Kwa hiyo tunaenda kuwa makini na timu hiyo kwani kila inapokuwa na morali inakuwa timu hatari na kuhusu wachezaji wanao wachezaji wakigeni wenaye Luis ni mchezaji mzuri nakumbuka nilimsajili kutoka Msumbiji na kumpeleka Simba kwa mkopo kabla".

"Ndio wakati niko Sundowns tulimtoa kwa mkopo hapa kiukweli ni mchezaji mzuri Sana na anafurahia kucheza mpira".

"Tunajua tunacheza dhidi yake na tinacheza na timu nzuri na hata katika ushambuliaji iko vizuri yule namba saba yuko vizuri, na hata yule namba 14 naye yuko vizuri na mchezaji mkubwa sana".

"Kwa hiyo tunajua kuwa hata katika viungo wao wapo wachezaji kutoka Zambia kifupi tunajua tunao wachezaji wazuri ili kucheza na timu nzuri". alisema Pitso Mosimane