
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), imeutangazia umma kuwa, Serikali imefanya mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya utozaji wa kodi ya majengo, sura 289, kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2023, ambapo viwango vya utozaji kodi hiyo vimebadilika, pamoja na wigo wa ukusanyaji umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo yote ya Wilaya.
.
Mamlaka hiyo imesema kodi hiyo itaendelea kutozwa kupitia ununuzi wa umeme (LUKU), ambapo nyumba ya kawaida iliyokuwa ikitozwa Tsh. 12,000/= kwa mwaka sasa itatozwa Tsh. 18,000/= kwa mwaka sawa na Tsh. 1,500/= kwa mwezi.
.
Aidha nyumba za ghorofa katika maeneo ya Majiji , Manispaa na Halmashauri za Mji zilizokuwa zikitozwa Tsh. 60,000/= kwa kila sakafu sasa zitatozwa Tsh. 90,000/= kwa kila sakafu, kwa mwaka sawa na Tsh. 7,500/= kwa mwezi.

