Back to top

Koromije waomba gari ya kubebea wagonjwa.

28 March 2022
Share

Wakazi wa kata ya Koromije wilayani Misungwi mkoani Mwanza wameiomba serikali na wadau wa maendeleo kuwasaidia upatikanaji wa gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha kata hiyo ili kupunguza athari ambazo zimekuwa zikijitokeza na kusababisha vifo hasa vya akina mama wajawazito wanaohitaji kusafirishwa kwenda maeneo mengine kupatiwa huduma.