Back to top

Kortini kwa tuhuma za kumpiga mwanae na kumchoma makalio.

27 February 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limefikisha mahakamani mtuhumiwa Mayaya Maduhu 32 mkazi wa kijiji cha Sagata wilayani Itilima mkoani Simiyu kwa la kumpiga na kumsababishia majeraha ya kudumu,mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu,aitwaye Nkamba Mayaya.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza leo ambapo akimsomea shtaka hilo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Bariadi Mary Mrio wakili wa serikali wa mkoa wa Simiyu Amani Abdalla,Hakimu amesema mshitakiwa huyo anatuhumiwa kwa kosa la kumpiga fimbo na kummwagia maji ya moto sehemu za makalio ,mtoto wake na kumsababishia  majereha ya kudumu.