Back to top

Kushuka uzalishaji zao la korosho matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu

13 September 2020
Share

Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Naliendele imesema elimu ya uzalishaji wa zao la Korosho bado ni changamoto kwa wakulima kutokana na wadudu wasumbufu wa magonjwa na matumzi yasiyo sahihi ya viuatilifu kuchangia uzalishaji wa zao hilo kushuka.

Akizungimza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kilimo bora cha Korosho wakulima wa zao hilo pamoja na maafisa ugani kutoka mkoa wa Mtwara mtafiti kutoka kituo cha utafiti tari naliendele Dadly Majune amesema changamoto ya ukosefu wa elimu ya uzalishaji bora wa zao la korosho umepelekea uzalishaji wa zao hilo kushuka.

Amesema msimu wa mwaka 2018/2019 takwimu zinaonesha kuwa uzalishaji ulipanda na kufikia tani laki tatu lakini msimu wa mwaka 2019/2020 uzalishaji umeshuka na kufikia tani laki mbili na elfu 32.

Amesema hali hiyo imepelekea taasisi ya TARI kutoa elimu ya uzalishaji bora wa zao la korosho ikiwemo kutambua magonjwa yanayosumbua zao hilo na madawa yanayotumika kuthibiti, lakini pia matumizi sahihi ya viwatilifu ili uzalishaji wa zao hilo uweze kuongezeka.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wameshkuru mafunzo hayo ambayo wamedai yataleta mafufaa makubwa katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo nchini.