Back to top

LEMA na GAMBO wamaliza tofauti zao za muda mrefu.

13 April 2018
Share

Mbunge wa Arusha  Mjini, Mheshimiwa GODBLESS LEMA na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bwana MRISHO GAMBO wamemaliza tofauti zao za muda mrefu.

Baadhi ya wananchi wamesema hatua hiyo itatoa fursa ya kuunganisha nguvu zao kushughulikia masuala ya maendeleo na kutatua kero zinazoikabili jamii.

Viongozi hao wamekutana ana kwa ana na kupeana mikono katika hafla ya uzinduzi wa Benk ya Stanbic, tawi la Arusha ambapo  licha ya kila mmoja kutambua nafasi ya mwenzake, walipopata nafasi ya kuzungumza, wote walijielekeza kuzungumzia masuala  ya maendeleo ya wananchi tofauti na ilivyokuwa awali walitumia muda mwingi kulaumiana na kulumbana.

Kwa muda mrefu sasa uhusiano na hata ushirikino kati ya Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Mheshimiwa GODBLESS LEMA na  viongozi na hata watendaji wa serikali umekuwa mdogo kutokana na tofauti za mitazamo na misimamo ikiwemo ya masuala ya   siasa.