Back to top

Siku ya Pasaka, wananchi watakiwa kusherehekea kwa amani.

04 April 2021
Share

Leo ni Pasaka, siku ambayo wakristo wanaadhimisha siku ya kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya kuteswa, kuuawa na kuzikwa.

Kitaifa, ibada ya Pasaka itafanyika katika Kanisa Katoliki parokia ya Msimbazi na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhahashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa limepiga marufuku sherehe za Pasaka badala yake limesema kilichopigwa marufuku ni matamasha na makongamano katika kipindi hiki cha maombolezo ya kitaifa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania David Misime akizungumza jijini Dodoma amewataka wananchi washerehekee kwa amani na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One na wafanyakazi wote wa kampuni hizo wanawatakia wananchi wote Heri ya Pasaka.