Back to top

Lissu akiwa Rais kuwafuta machozi wakulima wa zao la Pamba.

15 October 2020
Share

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu, ameingia mkoani Simiyu kuomba kura, huku akiwataka Watanzania kutumia muda wa siku 12 zilizosalia kabla ya zoezi la kupiga kura, kufanya uamuzi wa busara kwa maisha yao kwa kuwachagua wagombea wa Udiwani, Ubunge na Rais wanaotokana na chama hicho.

Wananchi wa mji mdogo wa Lamadi wilaya ya Busega, walifunga barabara kuu ya Mwanza - Musoma, wakati mgombea Urais huyo wa CHADEMA Mhe.Tundu Lissu alipokuwa akipita kuelekea Bariadi na maeneo mengine ya wilaya za Itilima na Meatu mkoani humo kuendelea na mikutano yake ya kampeni za uchaguzi mkuu.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu

Akiomba kura kwa wananchi wa Bariadi katika uwanja wa Mnadani, mgombea Urais huyo ameahidi kurejesha heshima ya wakulima wa zao la pamba wa maeneo hayo.

Katika mji wa Lagangabilili makao makuu ya wilaya ya Itilima, Kisesa pamoja na Mwanhuzi wilayani Meatu, ahadi ya mgombea huyo  Mhe.Lissu iwapo atapata ridhaa ya kuwa rais wa awamu ya sita, itakuwa ni kudumisha Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.