Back to top

Lissu ashindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi mbili zinazomkabili.

30 July 2020
Share

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi mbili miongoni mwa kesi zinazomkabili mahakama hapo ambazo zimepangwa kusikilizwa Agosti 26.

Awali Wakili upande wa utetezi Peter Kibatala aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Kupanga tarehe nyingine na kuieleza mahakama hiyo kuwa Lissu alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu  na alishauriwa kupumzika kutokana  na hali yake.

Upande wa Mawakili wa Jamhuri bila pingamizi wamekubaliana na pendekezo la kesi zote mbili ya kesi hizo kusikilizwa Agosti 26 mwaka huu.

Lissu amerejea nchini Julai 27 mwezi huu ikiwa ni miaka mitatu tangu alipoondoka mwezi wa tisa mwaka 2017 kwenda nchini Ubelgiji kufanyiwa matibabu hivi karibuni.

Kesi ya kwanza namba 123 ya mwaka 2017 tarehe 11 mwezi wa kwanza mwaka 2017 katika eneo la Kombeni mkoa wa  mjini Magharibi visiwani Zanzibar Tundu Lissu anadaiwa kutoa maneno ya kuumiza hisia za kidini.

Kesi nyingine ni  namba 236 ya mwaka 2017 katika eneo la Ufipa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam anayodaiwa kutoa maneno ya kichochezi.