Back to top

Lissu kurejesha utawala wa majimbo ili kutoa uhuru kwa wananchi.

18 September 2020
Share

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu amesisitiza umuhimu wa kurejesha utawala wa majimbo ili kutoa uhuru kwa wananchi kujiamulia mambo yao kwa kutumia raslimali zinazowazunguka.

Akihutubia maelfu ya wananchi wa Mji wa Mpanda katika Uwanja wa Kashato, mgombea urais huyo wa CHADEMA amekosoa kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt.Bashiru Ally kuhusiana na sera ya majimbo ambayo CHADEMA inainadi kwa Watanzania.

Aidha Lissu amesema akichaguliwa kuingia madarakani baada ya tarehe 28 mwezi ujao atakuwa Rais bora ambaye atasimamia uhuru, haki na maendeleo ya watu.

Mgombea Urais huyo akiwa njiani k wenda Mpanda kutokea mjini Sumbawanga amefanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Chala jimbo la Nkasi Kusini, Kalando jimbo la Nkasi Kaskazini na Majimoto jimbo la Kavuu.