Back to top

Lori lagonga magari manne,mtu mmoja afariki wanne wajeruhiwa Mbeya.

21 July 2020
Share

Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa baada ya lori la mizigo lililokuwa limebeba mbolea likitokea jijini Dar es salaam kwenda Zambia kufeli breki katika mteremko mkali wa mlima Mbalizi mkoani mbeya na kugoga magari mengine manne na bajaji moja kabla ya kupinduka.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 4 asubuhi ikihusisha lori lenye namba za USAJILI T 952 DJZ likiwa na tela T 277 BNN kufeli breki na kuyaparamia magari mengine manne na bajaji moja ambapo mwanamke mmoja aliyekuwa abiria kwenye bajaji amepoteza maisha papo hapo.

Kikosi cha Zimamoto na uokoaji kimefika eneo la ajali kutoa msaada kwa majeruhi na kufanya usafi ili barabara hiyo iendelee kupitika.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Sebastian Mbuta amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo .