
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, limekamata lori aina ya FUSO, lenye namba za usajili T 301 DPG, linalovuta tela lenye namba za usajili T 562 DNZ, mali ya kampuni ya K.T. ABRI, lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Mkoani Dar es Salaam, baada ya kukutwa likipakia magunia ya dawa za kulevya aina ya bangi 28, sawa na kilo 430, ambayo yalichanganywa pamoja na viroba 350 vya chakula cha kuku, katika Kijiji cha Mangae, mkoani humo.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama , amesema wanaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alikimbia na kulitelekeza lori hilo mara tu baada ya kubaini kuwa anafuatiliwa.
.
Pia Kamanda huyo amesema wamekamata pikipiki 6, zilizokuwa zikisafirisha magunia hayo ya bangi kutoka porini hadi kwenye eneo hilo ambapo waendesha pikipiki hizo nao wamekimbia.
