Back to top

LUCA MODRIC KUSALIA MADRID HADI 2024

26 June 2023
Share

Kiungo wa kati wa Croatia, Luka Modric amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utamfanya kuendelea kuwepo Real Madrid hadi 2024.
.
Mchezaji huyo mwenye umri miaka 37, ambaye alikuwa akihusishwa na kuhamia Ligi Kuu ya Saudi Arabia wakati mkataba wake ulipokuwa ukielekea mwishoni, ameichezea Real Madrid, mechi 488, huku akifanikiwa kushinda mataji matatu ya La Liga na Ligi ya Mabingwa mara tano, tangu atue kutoka Tottenham mwaka 2012.