Back to top

Lukuvi ataka wakurugenzi nchi nzima kukusanya kodi ya pango la ardhi.

26 February 2021
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi amewataka wakurugenzi nchi zima kuhakikisha wanakusanya kodi ya pango la ardhi kwa wakati kwa waliowamilikisha ardhi akisisitiza kuwa watauchukulia hatua mkoa wowote ambao utakuwa nyuma.

Mhe.Lukuvi ametoa agizo hilo baada ya kukabidhi hati ya hekari 75.29 ya shamba namba 97 katika eneo la luguruni kibamba kwa Manispaa ya Ubungo ikiwa ni utekeleza agizo la Mhe.Rais alilotoa tarehe 24 kwa wizara hiyo kukabidhi hati kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo ifikapo leo Ijumaa baada ya ombi kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kibamba.

Akizungumza baada ya kukabidhi hati hiyo Mhe.Lukuvi amesisitiza umuhimu wa viongozi kutekeleza maagizo ambapo ameutaka uongozi wa Manispaa hiyo kumpatia mchoro wa mipango ya mambo ya umma waliyopanga kuyafanya katika eneo hilo.