Back to top

Maafisa uhamiaji feki wakamatwa Kagera

26 June 2020
Share

Idara ya uhamiaji mkoani Kagera kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mashule kilichoko katika kata ya Kyamulaile ,Halmashauri ya wilaya ya Bukoba imewatia mbaroni Joseph Mugisha na Mohamed Shaban waliokuwa wakisakwa kwa tuhuma ya kujipatia fedha kwa kujifanya maofisa wa idara hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Afisa Uhamiaji mkoani humo Mrakibu Mwandamizi Thomas Fussy amesema watu hao walikamatwa Juni 21, mwaka huu majira ya saa nne usiku wakati wakijaribu kuomba fedha kiasi cha shilingi 500,000 kutoka kwa raia wa Uganda aliyemtaja kwa jina la Samwel Kalumba aliyekuwa akiishi kinyume na taratibu kwenye kijiji hicho ambaye pia anashikiliwa.