Back to top

Maagizo kwa Halmashauri, ujenzi wa madarasa.

23 November 2021
Share

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amezitaka halmashauri zote nchini ambazo zinatekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojulikana kwa jina la fedha za ustawi wa maendeleo na mapambano dhidi ya Uviko 19 kujenga kwa kuzingatia ubora na thamani ya halisi ya fedha kuendana na maagizo ya mheshimiwa Rais  Mama Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa.

Hayo ameyasema akikagua uienzi wa madarasa 26 katika wilaya ya Songwe mkoa wa Songwe kuona utekelezaji wa fedha zilizotolewa na serikali ili kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa nchini kabla ya kuanza kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwakani.

Aidha Naibu Waziri Silinde amezitaka halmashauri ambazo bado zipo nyuma katika ujenzi wa madarasa hayo kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kufunga taa wakati wa usiku ili kukamilisha ujenzi ifikapo Disemba 15 mwaka huu na kuwapongeza viongozi wa wilaya ya Songwe ambao wamejiongeza kufunga taa baadhi ya shule ili wajenge usiku na mchana waweze kukamilisha kwa wakati.