Back to top

Mkulima mwenye ulemavu aomba msaada alime kilimo chenye tija.

12 September 2020
Share

Ili kumsaidia  piga namba hii..0676 301 884.

Aron Ponera mtanzania mwenye ulemavu mkazi wa kijiji cha Mpitimbi wilayani Songea mwenye familia ya watoto watano  licha ya ulemavu wake lakini anajishughulisha na shughuli za kilimo hivyo amewaomba wasamaria wema na serikali kumsaidia ili alime kilimo chenye tija.

Ponera anasafiri kwa msaa  manne kutoka kijiji cha Mpitimbi kwenda Kitongoji cha Mashambani cha Mbwambwasi anakolima mashamba yake ambapo katika mashamba yake amelima maharage robo ekari kwa mkono wake na pia mwaka jana alilima mahindi hivyo anaomba yeyote mwenye mapenzi mema amsaidie.

Mke wa Bw. Ponera Bi. Anastazia Komba anasema familia ya watoto watano na yeye na mume  wake jumla saba inakuwa shida kwa mume wake kuweza kumudu kuihudumia.

Yeyote atakayeguswa na maisha ya Bw. Ponera  na kuhitaji kumsaidia awasiliane nae kupitia namba 0676301884.